Thursday 24 January 2008

PENDO LA GHIBU

1.moyo umefunga penzi, la mahabubu fulani

keshapo ninalienzi, lisidondoke changani

wanijiliapo wezi, huwa mfarakanoni

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



2.hapata wivu wa nafsi, nikaungua rohoni

nikabanguliwa rasi, ugonjwa nisibaini

tabu zisizo kiasi, kuninahili moyoni

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



3.mapenzi haya ya ghibu, kuwa kwake siamini

yalianza taratibu, kuingia akilini

sasa ndo nahisi tabu, mapenzi kunitahini

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



4.awali lihisi tamu, na furahiko ndotoni

hatekenya milizamu, nilalapo kitandani

kumbe najinywesha sumu, ya teseko maishani

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



5.akija huchekacheka, na kudekewa mwilini

pwani tukarukaruka, mfano mahayawani

sabahi kikurupuka, pekee hajibaini

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



6.ana uso wa duara, huburudisha aini

na kifua cha kufura, mwenyezi hakumhini

miguu ilo imara, hufurahisha machoni

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



7.ana macho ya kung'ara, mithali yake sioni

kope zake zimechora, mfano wa asumini

na libasi za sitara, kama zatoka peponi

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



8.nimekwenda kwa waganga, zindiko kulibaini

mitishamba kunisinga, kama mwari mafundoni

hirizi wakanifunga, kuenea maungoni

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



9.kila jambo halikuwa, ndugu nisaidieni

vitabu nimebukuwa, vya uchawi na vya dini

nimebaki naungua, mola hanipi idhini

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo



10.wakatabahu shairi, wajuvi nielezeni

kwa wale wanofasiri, ruwiya za mapenzini

naomba yenu nadhari, asaa nimbaini

ajabu moja ni kuwa, simjui mja huyo

Wednesday 23 January 2008

LADHA YA USHAIRI

AKILI KUZIHARIBU

1.wapungufu wa akili, kisha tunaziharibu
kwa maji yalo dhalili, twaadhirika ajabu
wasomi wenye adili, vileo huwatulubu
pombe hutudhalulusha, na kurufaisha akili

2.kwa zetu mbaya fiili, mola anatuadhibu
makatazo hatujali, tu wima kama bawabu
mwisho wa siku twafeli, peponi twajitanibu
pombe hutudhalilisha, na kurufaisha akili

3.twazitia uasili, amali ziso adabu
vinywaji vyenye mushkeli, twaviita vya mababu
mawazo ya kibaghili, viumbe yametusibu
pombe hutudhalilisha, na kurufaisha akili

4.wa moja hashiki mbili, ya busara na ulabu
ubongo hatuujali, hulegeza sukurubu
nyoyo hupata ajali, tukawa kama mabubu
pombe hutudhalilisha, na kurufaisha akili

5.himila wanohimili, bure hujitia tabu
hufura yao miili, na nyuso kufanya gubu
mtoto akiwasili, wakunga huwatulubu
pombe hutudhalilisha, na kurufaisha akili

6.nawaasa kula hali, mtenzi nawaadibu
kwa uchache wa kauli, penye makosa natubu
natetea maadili, siandiki kwa ghadhabu
pombe hutudhalilisha, na kurufaisha akili

MAISHA
1.maisha yanatutesa, na kutunyima huruma
hupatwa na vingi visa, kwa chukizo na hujuma
wengi hupata garasa, hata wanapojituma

2.maisha yana mikasa, kila siku kila juma
dunia hutikisika, kwa dhambi zenye kuuma
kama tulo na darasa, matusi tunavyosema

3.maisha yana makosa, mwanadamu hana jema
kama tulo na ruhusa, kwa vitendo vya uchama
tena hayo yote tisa, kumi kumtusi mama?

4.maisha yana usasa, cha zamani siyo chema
mcha mungu hukutesa, kwa kuwarudisha nyuma
ukihudhuria kesa, na fedha hukuazima

5.maisha yana anasa, akili usipotuma
vitamu hutovikosa, madhambi ukiyachuma
mwisho wale vibubusa, hulia na kuchutama

UTUMWA WA MAOVU
1.utumwaji wa maovu, hudhihaki milizamu
hukomaa kama kovu, ridhio lake ni hamu
moyo hupata machovu, na kulia madhulumu
ila mtumwa wa dhambi, hutubia akaacha

2.ovu halina utuvu, hufanya mwenye nidhamu
keshapo hushika shavu, kulia kibahaimu
akidai maonevu, yeye yamemstakimu
ila ajabu ya mungu, kesho hurudia tena!

3.hana ustahamilivu, muovu akikasimu
humnasa kama wavu, ubaya kwa wanadamu
tena huwa ni shupavu, hata jambole litimu
hapo hupata wasaa, akamkumbuka mungu

4.watovu wa usikivu, wovu washikwapo hamu
hupatwa na maumivu, katika zao fahamu
hawawi ni wakatavu, hudhani ni isilamu
hawaombeleki dua, nyoyo zimepigwa chapa

5.na hivi vina vya VU, vinaninyima kalamu
mfano wake VVU, umuri kunidhulumu
hapa nafanya kitovu, nimezidiwa elimu
vina vimeniishia, shairi laendelea.

Sunday 20 January 2008

taaluma ya uandishi wa habari

taaluma ya uandishi, imejitokeza
ni kazi ya aushi, yapendeza
wachukiao ni wabishi, tutawabeza
karibuni tanzania, uandishi unangaa

urembo

urembo tanzania, unapendeza

kwa wote wenye nia, vema kujitokeza

kwa kheri na taania, tutawapongeza

Saturday 19 January 2008

mashairi ya kido

kuanzia sasa jiandae kupata mashairi mapya, kila mungu ataponijaalia kuklaa katika ngamiza na kuandika nilichojaaliwa kwa siku hiyo. kwa leo anza na hili shairi dogo...



GOD OF MANY COLOUR



my father use to tll me

God is one

Wasn't born

and all alone



But now aday's

People lost

They almost

like ghost



Every group have God

who named

Always instead

By race and colour



Who is the real one

I want to follow

Before him to bow

ooh!!.. my mind allow



The God of many colour

I'm with you

White, Black or Blue

They praise your name







LOVE IS.....



Love is every where

it exist

For one who care

can't resist

And those who aware

fail at last



I always pray to God

to get one

Who will raise my mood

being fine

ooh!! yes i understand

love is line



Many people tend to cry

for love

make their soul fly

to deserve

but most of them lay

to achieve



I lost my cute GRACE

for jelous

I have no one to replace

it's dangerous

Her eyes was like spice

ooh!! hopelesness



Now im all alone

I cry!

Everything i concern

now it fly

The tears it drown

cant dry!







PESA SUMU



pesa sumu ya furaha, ila huleta mapenzi

waliokosa shabaha, huniona mpuuzi

ajabu nao huhaha, kuwaridhisha vipenzi

dunia yetu ya sasa, bila pesa hupendeki



ajabu ya jambo hili, halipati magunduzi

wengi tunastahamili, na nyoyo kupata ganzi

hudhani tunastahili, kwa udhati wa mapenzi

kupenda hakutoshi kitu, watu wanataka pesa!



pendo hapewi baghili, nimefanya uchunguzi

wake wana maufili, na waume ni washenzi

mapenzi yenye adili, kuyapata hatuwezi

mmoja akiwa mwema, wa pili huharibika



mapenzi janga la kiu, na hilo ni toka enzi

mtoa ana dharau, hafikirii ijazi

mpokea ni bahau, mchafu mwenye kutuzi

al-khitaju hanitha, lau kanna rijaalu..



wakatabahu bakungwi, ni mwisho wa maongezi

ajifaae hanangwi, hupata mambo azizi

mapendo ni kama mwangwi, kuuzuia huwezi

na kazi ipo kwa yule, mpenda asiependwa





PUMZI



pumzi zina hadaa, na kutupa kiburi

tena bila ridhaa, ya mola maamuri

nyoyo zimetufubaa, hatuogopi kaburi



maudhi na shufaa, hupeleka umuri

mengi yasiyofaa, hupulizwa uturi

unyonge na zanaa, waja hayawaghuri



dunia kama jaa, kawaida si zuri

taka zisizofaa, ndiwo huu umuri

maisha ni kichaa, waja hatufikiri



wevi wa makataa, husubiri kujiri

hawangoji ridhaa, kukutia kabari

wangeiba asaa, hutukata umuri!!!..

Friday 18 January 2008

ushairi Tanzania

naanza kwa maamkizi ya kitanzania, wakubwa shikamooni na wadogo wa makamo yangu habari za leo.

ushairi ulianza karne nyingi zilizopita, lakini fasihi kwa ujumla ilianza tangu kutambulika kwa lugha. nami naamini kuanza kuwepo wakaazi ndani ya tanzania ambapo awali ikitambulika kama Tanganyika na sitambui kabla ya Tanganyika ilikuwa ikitambuliwa kwa jina gani, maana twaambia na historia kuwa jina hili Tanganyika lililwetwa na wakoloni.

kazi za kijamii ndizo zilizoivumbua sanaa ya ushairi hasa, kadhalika mambo ya kiutawala na unyonyaji ndivyo vilivyokuja kuiendeleza na kuitilia vidoko sanaa hii. ingwa wapo watu waso fikira wala uzalendo wanaodiriki kusema kuwa sanaa ya ushairi ililetwa na waarabu. mawe!.. kamwe sikubaliani na ukweli huu.

ushairi ni wa kale, anaebishana aje

tangu wana na wavyele, lugha yetu waitaje

sikizeni kwa makele, tabia msinifuje

mkadai ni mtovu, historia kuipinda



hicho ni kitambulisho changu tu katika blogu hii, nina muda mchache sana wa kukaa na ngamiza, wakoloni wanaiita 'computer'. hivyo kunifanya kuwa na kauli ndogo na ulimi mfupi usokidhi matakwa ya wasikizaji na wasomaji wangu, poleni kwa hilo.

lakini mungu akinipa uhai na afia njema nitauendeleza mjadala huu kwa mifano hai na marejeo mema ya waandishi walowahi kuingia katika mjadala huu mzito mpaka mungu akazirufaisha roho zao kwa kuzipeleka kusikorudi.

saadan S kandoro, alitaabika sana

kwa tungo na mishororo, pambo za beti na vina

kuwarudisha watoro, lugha waloitukana

na mapurofesa lukuki, wa BAKITA na TUKI

HAFIDH A.KIDO (TOTO LA BAKUNGWI)

SIMU 0713593894.

BOX 1256

TANGA -TANZANIA

19-10-2008(AD)

10-MFUNGO NNE-1429(AH)