Friday 18 January 2008

ushairi Tanzania

naanza kwa maamkizi ya kitanzania, wakubwa shikamooni na wadogo wa makamo yangu habari za leo.

ushairi ulianza karne nyingi zilizopita, lakini fasihi kwa ujumla ilianza tangu kutambulika kwa lugha. nami naamini kuanza kuwepo wakaazi ndani ya tanzania ambapo awali ikitambulika kama Tanganyika na sitambui kabla ya Tanganyika ilikuwa ikitambuliwa kwa jina gani, maana twaambia na historia kuwa jina hili Tanganyika lililwetwa na wakoloni.

kazi za kijamii ndizo zilizoivumbua sanaa ya ushairi hasa, kadhalika mambo ya kiutawala na unyonyaji ndivyo vilivyokuja kuiendeleza na kuitilia vidoko sanaa hii. ingwa wapo watu waso fikira wala uzalendo wanaodiriki kusema kuwa sanaa ya ushairi ililetwa na waarabu. mawe!.. kamwe sikubaliani na ukweli huu.

ushairi ni wa kale, anaebishana aje

tangu wana na wavyele, lugha yetu waitaje

sikizeni kwa makele, tabia msinifuje

mkadai ni mtovu, historia kuipinda



hicho ni kitambulisho changu tu katika blogu hii, nina muda mchache sana wa kukaa na ngamiza, wakoloni wanaiita 'computer'. hivyo kunifanya kuwa na kauli ndogo na ulimi mfupi usokidhi matakwa ya wasikizaji na wasomaji wangu, poleni kwa hilo.

lakini mungu akinipa uhai na afia njema nitauendeleza mjadala huu kwa mifano hai na marejeo mema ya waandishi walowahi kuingia katika mjadala huu mzito mpaka mungu akazirufaisha roho zao kwa kuzipeleka kusikorudi.

saadan S kandoro, alitaabika sana

kwa tungo na mishororo, pambo za beti na vina

kuwarudisha watoro, lugha waloitukana

na mapurofesa lukuki, wa BAKITA na TUKI

HAFIDH A.KIDO (TOTO LA BAKUNGWI)

SIMU 0713593894.

BOX 1256

TANGA -TANZANIA

19-10-2008(AD)

10-MFUNGO NNE-1429(AH)

No comments: